Mtandao wa Ethereum ndio ulikua wa kwanza kutumia huu muundo wa kuhakikisha hesabu zake zinafanyika kutumia uhakikishaji wa umiliki wa sera za Ethereum(ETH).
Katika mitandao ya bloku mfumo sera za crypto za kienyeji za hii mitandao zina dhibitiwa na mtu/kikundi ama kampuni ambazo zina tarakilishi zilizo na uwezo maarufu wa kufanya hesabu ngumu ya hizi mitandao.
Katika huu muundo wa umiliki wa sera za crypto katika kutenda kazi za bloku mfumo,inamaanisha ya kwamba ndio uweze kuhifadhi rekodi na kuhakikisha sera za crypto zimewekwa vizuri lazima uwe na kiwango fulani cha hizo sera.
Kisha ukiwa na hizo sera unaweza kwa kutumia programu za tarakilishi zinazo hakikisha ya kwamba shughuli zote za kutuma ama kupokea sera za crypto zinafanyika vile zinahitajika katika huo mtandao.Ukifanya hii shughuli unapata malipo kwa njia ya sera za crypto za kienyeji za huo mtandao.
Hii mbinu ya kutumia sera za mtandao fulani unazo miliki ndiposa uweze kuhakikisha fedha za crypto zinatumwa na kupokewa katika huo mtandao jinsi zinavyofaa na kisha kupata malipo unaitwa hakikisho la umiliki katika utenda kazi wa crypto(proof of stake).