Je ushahidi wa utekelezaji wa kazi (proof of work) ni nini ?

Apr 28, 2022 1 min read
Je ushahidi wa utekelezaji wa kazi (proof of work) ni nini ?

Katika mitandao ya bloku mfumo sera za crypto za kienyeji za hii mitandao zina dhibitiwa na mtu/kikundi ama kampuni ambazo zina tarakilishi zilizo na uwezo maarufu wa kufanya hesabu ngumu ya hizi mitandao.
Hizi hesabu ambazo zinafanywa na hizi mitandao zina hakikisha ya kwamba mtu yeyote anaye tuma ama kutumiwa sera za huo mtandao anaweza kupokea na kutuma.Hii ni kumaanisha ya kwamba kabla haujatuma sera zozote ukona hizo sera kwa akaunti yako na pia anaye zipokea pia amezipata kwa akaunti yake.Hii rekodi ya shughuli ya kutuma na kupokea hizo sera inarekodiwa na kutangazwa kwa tarakilishi zingine kwa huu mtandao wa bloku mfumo.

Rekodi zote za kutuma ama kupokea sera za crypto zinahifadhiwa katika bloku ambazo zinapangwa kulingana na hesabu iliyotengenezwa na walio unda huo mtandao.

Tarakilishi ambayo inaweza kufanya hii hesabu kwa haraka zaidi na kuongeza hizo rekodi kwa bloku inazawadiwa vipeni vya crypto vya huo mtandao,kwa mfano kama ni Bitcoin hiyo tarakilishi inazawadi kiwango fulani.Hii ni kumaanisha wenye tarakilishi ndio watakua wamezawadiwa.

Na kwa sababu hizi tarakilishi ziko kila pahali duniani haiwezekani kuzuia ama kufunga mtandao huu.Na pia inamaanisha hakuna tarakilishi moja ama vikundi vyake vinaweza kudhuru hii oparesheni kwa sababu zinahitaji ziwe na zaidi ya 51% ya nguvu ya tarakilishi zingine zikiunganishwa kwenye huo mtandao.

Hizi shughuli za tarakilishi tofauti kuweza kufanya hii hesabu na kuongeza rekodi katika bloku mfumo kwa kusuluhisha hesabu tata ya huo mfumo wa bloku kisha kuzawadiwa na vipeni vya kienyeji vya huo mtandao ndio inaitwa ushahidi wa utekelezaji wa kazi(proof of work).Umepewa hii jina sana sana kwa sababu inahusu kusuluhisha hesabu maalum kabla ya kuongeza hiyo rekodi kwa bloku na kuitangaza kwa tarakilishi zingine.

Great! Next, complete checkout for full access to Stake DAO Academy.
Welcome back! You've successfully signed in.
You've successfully subscribed to Stake DAO Academy.
Success! Your account is fully activated, you now have access to all content.
Success! Your billing info has been updated.
Your billing was not updated.