Unaweza nunua na kuuza aje sarafu za crypto ?

Apr 12, 2022 1 min read
Unaweza nunua na kuuza aje sarafu za crypto ?

Unaweza nunua na kuuza aje sarafu za crypto

Unaweza kununua na kuuza sarafu za crypto kutoka kwa soko za sarafu za crypto mtandaoni.

Kuna aina mbili za soko ,kuna zile ambazo zina simamiwa na kampuni binafsi na zile ambazo hakuna kampuni binafsi inayosimamia ila ni programu za tarakilishi zinazo simamia.

Zile soko zinazo simamiwa na kampuni binafsi zinawapa wauzaji akaunti za kuuza na kununua na zinawapa uwezo wa kupata neno siri tena la akaunti yao wakipoteza ama kusahau.
Lakini mara mingi haiwapei wauzaji ama wanunuzi uwezo wa kupata maneno ya siri ya pochi zao yanayo wapa idhini ya kutumia sarafu za crypto kutoka kwa bloku mfumo,kwa hivyo kila wanapo hitaji kuuza ama kununua lazima waende mtandaoni kwa ule tovuti(website) wa hii kampuni binafsi ndio waweze kutekeleza hicho kitendo.

Zile soko zinazo simamiwa na programu za tarakilishi zikona algorithm ambayo ina hakikisha ya kwamba mtu anaye uza ama kununua atapata bei inayo faa na hakutakua na vitendo vya ulaghai vinavyo wezekana.Hii soko huwapa watumizi wake bei njema zaidi na uwezo wa kuhifadhi maneno yao ya siri yanayo wapa idhini ya kutumia sarafu zao za crypto kutoka kwa bloku mfumo.

Kabla haujaanza kununua na kuuza ni vizuri kujua umuhimu wa hizi soko ndipo uweze kuchagua inayo kufaa.

Great! Next, complete checkout for full access to Stake DAO Academy.
Welcome back! You've successfully signed in.
You've successfully subscribed to Stake DAO Academy.
Success! Your account is fully activated, you now have access to all content.
Success! Your billing info has been updated.
Your billing was not updated.