Tofauti ya hizi mitandao zisizo unganika na zilizo unganika ni kwamba kwa hizi mitandao hakuna mtu/watu ama kampuni binafsi iliyo na uwezo wa kuzuia ama kudhoofisha shughuli za ununuzi ama uuzaji wa sera za crypto.Katika hizi soko mnunuzi ama muuzaji wowote anaweza jumuika katika shughuli za biashara bila kuhitaji idhini kutoka kwa mtu mwingine ama kampuni yeyote inayo simamia hii soko.
Teknologia ya bloku mfumo yenyewe haina taasisi/mtu/watu wanaosimamia shughuli zake ila haya majukumu yamegawanyika kwa tarakilishi mbali mbali katika sehemu tofauti tofauti duniani.
Hii inawezesha teknologia hii kuweza kutumika bila uwezo wa kufungwa , kudhulumiwa ama kuzuiwa katika sehemu yeyote kwa sababu hakuna mtu mmoja ama serikali iliyo na idhini ama uwezo wa kufanya hivi vitendo.
Hivi hivi ndivyo soko za sera za crypto zisizounganika zina endeleza oparesheni zake bila mtu binafsi kuweza kuzima,kuzipa idhini,kuzidhuru ama kuzizuia.Hii inawezekana kwa sababu ya muundo wake unao fuata nyayo za muundo wa bloku mfumo.