Teknologia ya Bloku mfumo ni nini ?
Katika teknolojia ya Bloku mfumo (block chain) , data inapangwa katika vipande vinavyo fuata mfumo fulani , hivi vipande vinaitwa bloku.Hizi bloku zinaishi katika mtandao wa tarakilishi , kila wakati ambapo bloku mpya ya data inafanyika ,hiyo bloku inapangwa juu ya bloku iliyoko hapo awali.
Huu mfumo wa kuongeza bloku juu ya iliyokua hapo awali unasababisha kuwepo kwa mpangilio wa bloku za data moja baada ya nyengine,zikitengeneza mnyororo wa bloku za mfumo mmoja. Tarakilishi zote ambazo zinahifadhi huu mnyororo wa hizi bloku zina jukumu ya kuhakikisha ya kwamba data iliyoko kwa hizi bloku haijaharibika.
Ubora wa teknologia hii ni kwamba si tarakilishi moja inayodhibitisha data iliyo kwa hizi bloku kuwa sahihi ila ni tarakilishi nyingi zilizo kwenye mtandao.Hii inaifanya hii teknologia iwe na njia ya kuthibitisha uhakika isiyotegemea tarakilishi moja ila inategemea tarakilishi nyingi , vile vile inaifanya iwe ngumu kwa mtu yeyote kuweza kutumia tarakilishi moja kugeuza data iliyo kwenye huu mnyororo wa bloku za mfumo moja.
Uwezo wa teknolojia ya bloku mfumo ya kukua na data sahihi katika bloku inawezesha utengenezaji wa vipeni vinavyoweza kutumika kama pesa katika mtandao.Teknologia ya bloku mfumo (block chain) imeongezeka umaarufu miaka ya hivi karibuni sababu ya vipeni vyake (digital assets) vinavyotumika katika kukamilisha biashara tofauti katika mtandao.
Ubinafsishaji wa technologia ya bloku mfumo umesababisha aina nyingi za vipeni kuibuka katika vipeni vyote vilivyoko Bitcoin(BTC) na Ethereum(ETH) ndivyo vinavyo julikana zaidi.