Bitcoin(BTC) ni aina moja ya sarafu za crypto.Bitcoin ndiyo ilikua sarafu ya kwanza kubuniwa na kutumika katika kufanya biashara za mtandaoni.Hii imeiwezesha kukua na umaarufu wa hali ya juu zaidi ya sarafu zingine za crypto.
BTC ilitengenezwa na kikundi ama jamaa aliyekua anatumia jina Satoshi Nakamoto,kwa kuonyesha heshima na shukrani kwa hiki kikundi ama jamaa , kiwango kile kidogo kabisa cha BTC ambacho ni 0.00000001 kikaitwa Satoshi.
Mawazo yaliyo pendekeza kutengenezwa kwa Bitcoin(BTC) yanaweza patikana kwa karatasi nyeupe ya hiyo teknologia.
Mtandao wa Bitcoin(BTC) unatumia algorithimu inayoitwa Proof of Work(POW) ambayo ina hakikisha tarakilishi fulani katika huu mtandao wa bitcoin(Miners) zinatumia uwezo wa CPU zao kuhakikisha kila shughuli za mtandao inayohusu kutuma na kupokea BTC inafanyika vile inavyo paswa kufanyika.Hizi tarakilishi zinazofanya hii shughuli zinapata malipo ya BTC