Ethereum

Apr 14, 2022 1 min read
Ethereum

Ethereum ni mtandao unaotumia teknolojia ya bloku mfumo huu mtandao ulianzishwa mwaka wa 2015.Sarafu za crypto za mtandao wa Ethereum zinaitwa Ether(ETH) algorithimu ambayo inatumika kuhakikisha shughuli zote za huu mtandao zinaendelea vyema inaitwa Proof of Stake(POS),ambapo kila aliye na sarafu za crypto za aina ya Ether anaweza zisajili kwa mtandao ndio aweze kudhibiti shughuli zinazofanyika katika mtandao huo na kisha kupokea malipo kwa aina ya sarafu za Ether(ETH).

Mtandao wa Ethereum ulipata umaarufu kwa kukua mtandao wa kwanza kuwepo na uwezo wa kuweka mikataba kati ya sehemu tofauti tofauti za mtandao huo na kuwezesha shughuli zaidi ya kupokea na kutuma sarafu za crypto,hizi shughuli zilikua kuongezeka kwa uwekezaji wa ETH na kuwezesha kutumia ETH kutengeneza sarafu za crypto za kibinafsi.

Uwezo wa kutengeneza sarafu za crypto za kibinafsi ukitumia mtandao wa Ethereum kama msingi umesababisha kuwepo kwa aina mingi za programu zinazotumia hii teknologia ya bloku mfumo(decentralized applications).Tofauti moja kuu kati za mtandao wa Bitcoin na Ethereum ni kwamba katika mtandao wa Ethereum kuna uwezo wa kutengeneza sarafu za crypto za kibinafsi(tokens) ambazo unaweza tumia kufanya chochote utakacho kwa huo mtandao.

Great! Next, complete checkout for full access to Stake DAO Academy.
Welcome back! You've successfully signed in.
You've successfully subscribed to Stake DAO Academy.
Success! Your account is fully activated, you now have access to all content.
Success! Your billing info has been updated.
Your billing was not updated.