Aina za pochi za sarafu za crypto

Apr 12, 2022 1 min read
Aina za pochi za sarafu za crypto

Kuna aina nne za pochi za sarafu za crypto.

Pochi la tarakilishi hili ni lile pochi ambalo linatumika ndani ya tarakilishi,hili pochi lazima kwanza uweke programu yake kwenye tarakilishi yako ndio sasa uweze kulitumia.

Pochi la kutumika mtandaoni hili ni lile pochi ambalo linatumika katika kivinjari(browser) ndio uweze kutumia hii pochi unahitaji mtandao.

Pochi lililo tengenezewa kifaa chake , hizi pochi zinafanana USB.Ndio uweze kutumia hizi pochi lazima kwanza uunganishe kwa tarakilishi.Uzuri wa hii pochi ni kua unaweza ibeba pahali popote uendapo.

Pochi la karatasi hii ndio njia rahisi sana ya kuhifadhi sarafu za crypto hili pochi linahusu kuandika kwa karatasi majina ya siri ya pochi lako na kuyaweka pahali pema.Kila unapohitaji kutuma ama kufanya jambo lolote linalohusu sarafu za crypto unahitaji kukumbuka hayo majina ya siri alafu utapata nafasi ya kuyajaza kwa pochi lingine lolote kabla ya kufanya jambo lolote.Ubora wa hii pochi ni kua unaweza kutumia na pochi ya aina yeyote kwa zenye nimetajwa hapo awali.

Great! Next, complete checkout for full access to Stake DAO Academy.
Welcome back! You've successfully signed in.
You've successfully subscribed to Stake DAO Academy.
Success! Your account is fully activated, you now have access to all content.
Success! Your billing info has been updated.
Your billing was not updated.