Pochi za sarafu za crypto ni nini ?

Pochi za sarafu za crypto ni programu zinazosaidia kuhifadhi vipeni vya bloku mfumo

Pochi hizi ni tofauti sana na pochi zingine ziliwemo kwa njia moja kuu.
Hizi pochi za sarafu zina jukumu ya kuhifadhi , kutunza na kuthibitisha majina ya siri yanayo wezesha kutuma na kupokea sarafu hizi katika hilo pochi,haya majina ya siri ndiyo yanampa mtu idhini ya kufikia sarafu za crypto zilizo kwenye bloku mfumo.

Mtu yeyote anaye jua haya majina ya siri ya pochi lolote anapata mamlaka kamili ya kutawala lile pochi.Anaweza pokea fedha za crypto , anaweza tuma na pia kuthibitisha ujumbe akitumia lile pochi.Ndio sababu ni muhimu kuyatunza haya majina ya siri ya pochi unalolitumia kuhifadhi sarafu zako.

Hizi pochi uwezesha watumizi wa sarafu za crypto kutumia nenosiri ndio waweze kutumia hizi pochi bila kubidi wakumbuke majina ya kriptografia.

Kuna aina mbili za pochi, pochi iliyo unganishwa kwa mtandao na isiyo unganishwa kwa mtandao.

Kati ya hizi pochi mbili ni vizuri kutumia isiyo unganishwa na mtandao kama una sarafu mingi kwa sababu hii ndio iliyo salama zaidi.Lakini kama una kiwango kidogo cha sarafu za crypto na unatumia hizo hela mda kwa mda ni rahisi kutumia pochi iliyo unganishwa na mtandao.